Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 8 Februari, 2024 ametembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani zilizopo katika Jiji la New York na kupokelewa na Mwenyeji wake Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa nchini Marekani Mhe. Dkt. Suleiman Haji Suleiman.