Mhe. Balozi Suleiman H. Suleiman, Kaimu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa New York, leo tarehe 17 Julai 2025 amekabidhi kwa Mhe. Philemon Yang, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tafsiri kwa lugha ya Kiswahili ya Mkataba wa Zama Zijazo (Pact for the Future). Tafsiri ya Mkataba huo kwa lugha ya Kiswahili imetolewa kama mchango wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani kwa mwaka 2025. 

Katika ghafla hiyo Mhe. Philemon Yang alisema kuwa “Lugha si tu chombo cha mawasiliano bali pia ni njia ya ujumuishaji, umiliki na kuleta maendeleo”. Mkataba huo sasa upatikana katika lugha 33 ikiwemo Kiswahili, ukifikia watu zaidi ya bilioni 3.5 duniani. Hatua hiyo itarahisisha utekelezaji wake katika ngazi ya Kitaifa kwa kuwa watu wengi zaidi wataweza kuusoma na kuelewa kwa lugha zao. 

Mchango huo wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa utasaidia kuendeleza utaendelea kuchangiza kuenea zaidi kwa lugha ya Kiswahili na kuendelea kuipenyeza lugha hiyo kwenye Umoja wa Mataifa. 

Aidha katika ghafla hiyo, Mhe Yang, alizindua tovuti mahsusi ya Umoja wa Mataifa ambapo tafsiri ya Mkataba huo katika lugha mbalimbali itapatikana na kusomwa na watu wengi zaidi ulimwenguni katika siku zijazo.