Mkutano baina ya Mhe. Balozi Dr Suleiman Haji Suleiman Kaimu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa na Mhe.Balozi Abbas Kadhom Kaimu Mwakilishi wa Kudumu wa Iraq katika Umoja wa Mataifa New York wamekutana na kufanya mazungumzo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York tarehe 18 Julai 2025.

Mazungumzo yalikuwa na lengo la kuimarisha mahusiano ya Kindugu baina ya Tanzania na Iraq ,kukuza biashara baina ya nchi mbili hasa bidhaa za mazao ya chakula. 

Aidha, Iraq imeonyesha utayari wake wa kufungua tena Ofisi zake za Ubalozi nchini Tanzania.

Halikadhalika Iraq imekusudia kuifanya Tanzania kuwa HUB ya Biashara yake ya Mafuta kwa nchi za Mashariki Kati na Kusini mwa Afrika. 

Kwa niaba ya Serikali ya Iraq Balozi Abbas amezialika mamlaka za uwekezaji na Biashara za Tanzania kutembelea Iraq kwa ajili ya kujionea fursa za uwekezaji.