Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango amekutana kwa mazungumzo ya faragha (Tete a tete ) na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Antonio Guterres katika Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini New York tarehe 22 Septemba 2022.

Makamu wa Rais yuko nchini Marekani ambapo anatarajiwa kuhutubia Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaondelea nchini nchini humo.